Watu wasiopungua watatu wameuawa na wengine 17 kujeruhiwa
baada ya bomu la kutegwa garini kuripuka karibu na ubalozi mdogo wa Marekani
huko Herat Afghanistan.
Sayed Fazlullah Wahidi, Gavana wa jimbo la Herat
amesema shambulio hilo limetokea asubuhi ya leo ambapo bomu la kutegwa garini
lililipuliwa umbali wa mita 60 kutoka ubalozi huo.
Sauti ya mlipuko ilifuatiwa
na milio ya risasi ambapo askari polisi wawili na afisa usalama wa ubalozi huo
wameuawa huku watu wengine 17 wakijeruhiwa.
Msemaji wa kundi la Taliban
Qari Yousef Ahmadi ametangaza kuwa kundi hilo ndilo lililotekeleza shambulio
hilo.
Shambulio hilo limejiri ikiwa ni siku mbili tangu
wapiganaji wa Taliban wavurumishe makombora kadhaa katika kituo cha jeshi la anga
cha Bagram ambacho ni kituo kikubwa zaidi cha kijeshi cha Marekani nchini
Afghanistan.


0 comments:
Post a Comment