Image
Image

UNHCR: TANZANIA YAWAFUKUZA WARUDI 30,000.


Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa limesema kuwa maelfu ya Warundi waliokuwa wakiishi katika nchi jirani ya Tanzania wamerejeshwa nchi kwao kwa nguvu katika siku 30 zilizopita. 

Catherine Huck, Kamishna wa UNHCR amesema kwamba, ni vigumu kujua idadi ya Warundi waliofukuzwa kutoka Tanzania lakini kwa uchache ni watu kati ya elfu 20 hadi elfu 30.

Karibu Warundi milioni moja walivuka mpaka na kuingia Tanzania wakati wa vita vya ndani vya mwaka 1993. 

Ingawa wakimbizi wengi wa Burundi walirejea nchini kwao baada ya vita hivyo kuisha mwaka 2006 lakini baadhi yao bado wanaishi  nje ya nchi ikiwemo Tanzania.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment