Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amesisitiza kuwa kwa mujibu
wa sheria za kimataifa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ndio chombo pekee
kinachopaswa kufuatilia mgogoro wa Syria.
Akizungumzia mabadiliko yanayojiri
Syria, Zuma amesema, katika mkutano wa kundi la G20 uliofanyika huko Petersburg
nchini Russia nchi nyingi hasa wanachama wa kundi la Bricks zilipinga mpango wa
kushambuliwa Syria.
Zuma aidha ameongeza kuwa, Umoja wa Mataifa ndio mahali
bora zaidi pa kutatulia mgogoro wa Syria na masuala mengine yanayohusu usalama
wa dunia.
Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi duniani zilizopinga
waziwazi hatua ya Marekani ya kutaka kuishambulia kijeshi Syria.


0 comments:
Post a Comment