DAR/ZANZIBAR.
SIKU
moja baada ya Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, Mkoa wa Kusini Unguja,
Joseph Mwang’amba kumwagiwa tindikali na
watu wasiojulikana, imebainika kuwa alitishiwa kuuawa miezi mitatu kabla ya
kukutwa na tukio hilo.
Wakati
Padri huyo akieleza hayo, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, ameijia juu
polisi kwa kushindwa kudhibiti matukio ya viongozi wa dini na serikali visiwani
humo, kushambuliwa kwa kumwagiwa tindikali huku akilitaka kuwakamata
waliohusika na tukio hilo.
Kiongozi
huyo wa dini, aliyejeruhiwa maeneo ya usoni, mikononi na kifuani baada ya
kumwagiwa tindikali hiyo alisafirishwa jana na ndege ya kukodi ya Shirika la
Coastal kutoka visiwani humo hadi Dar es Salaam na baadaye kupelekwa Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.
Dk
Shein alisema Polisi inatakiwa kuongeza nguvu za uchunguzi ili kukabiliana na
matukio ya kikatili ya umwagaji wa tindikali, yanayoshamili visiwani humo hivi
sasa.
“Hatuwezi
kuviacha vitendo hivi viendelee … ni lazima Jeshi la Polisi lijitahidi kuwatafuta
wahusika ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Dk Shein.
Dk
Sheni alisema, kitendo hicho ni cha kikatili na kisichovumilika na kuongeza
kuwa wahusika lazima wasakwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa
upande wake, Padri wa Parokia ya Mtakatifu Joseph, Zanzibar, Thomas Assenga
aliyefuatana na kiongozi huyo mpaka MNH, alisema siku za nyuma Padri Mwang’amba
alitolewa vitisho na mtu ambaye hamfahamu wakati akienda kutoa huduma katika
kituo cha wazee cha Welezo.
Alisema
kabla ya kufika kituoni hapo, kuna eneo ambalo nyakati za asubuhi watu hufanya
mazoezi barabarani ambapo kuna mtu mmoja alimtolea maneno ya vitisho.
“Unajua
kawaida ya watu wa Zanzibar hufanya mazoezi barabarani, sasa kipindi anapita
eneo hilo katika kilima, kuna mtu alimwambia atamfanyia kitu kibaya ambacho
hatujui ndiyo hiki au la,” alisema Padri Assenga na kuongeza:
Alisema
Juni mwaka huu mara baada ya kupewa vitisho hivyo alikwenda kutoa taarifa kwa
Sheha wa eneo hilo na kituo cha polisi.
“Mara
baada ya kutolewa vitisho hivyo Juni mwaka huu, alichukua jukumu la kwenda
kutoa taarifa kwa mkuu wa eneo hilo (Sheha) na kituo cha polisi.”
Akielezea
tukio la kumwagiwa tindikali Padri Mwang’amba, alisema alimwagiwa saa 9:45
alasiri juzi wakati akizungumza na simu nje ya internet café iliyopo eneo la
Mlandege. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment