Vyama vya siasa vya
upinzani vya NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF vimekubaliana kuanzisha ushirikiano
wa pamoja na kuwa na msimamo mmoja juu ya mchakato wa uandikaji wa katiba mpya,
ambapo viongozi wa taifa wa vyama hivyo wametangaza kuupinga muswada wa marekebisho
ya sheria ya mabadiliko ya katiba wa mwaka 2013, uliopitishwa na bunge.
Viongozi wa vyama hivyo
wakizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam wamesema wanakusudia
kurejea kwa wananchi na kuainisha kile walichodai mikakati ya namna ya kupata
na kudai katiba mpya, ambapo Septemba 21 mwaka huu vitafanya mkutano mkubwa katika
viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam.
Miongoni mwa madai ya vyama hivyo vikuu vya upinzani
nchini kupinga muswada huo na kumwomba rais asiusaini, ni marekebisho hayo
kufanyika kinyume na maoni ya wadau, ikienda kinyume na makubaliano ya awali ya
kamati ya bunge ya katiba, sheria na utawala baada ya kupokea maoni ya wadau wa
Tanzania bara, kutoshirikishwa kwa upande wa pili wa muungano sambamba na kudai
muswada uliopelekwa bungeni uliongezwa vifungu vingi ambavyo havikuwemo katika
rasimu iliyopelekwa kwenye serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment