Jeshi la polisi
limeendelea na mpago wake wa kuhamasisha viongozi wa dini nchini kuanzisha
kamati za ulinzi na usalama kwenye nyumba za ibada ili kukabiliana na matukio
ya uvunjifu wa amani yanayotekelezwa na baadhi ya watu wachache wenye nia ovu
kwenye nyumba za kuabudia.
Mkuu wa Utawala wa Jeshi
la Polisi DCP Thobias Andengenye akizungumza wakati wa mafunzo kwa
viongozi wa kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Mashariki na pwani, juu ya unzishwaji wa kamati
hizo, amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha usalama unaimarishwa hadi kwenye ngazi
ya familia.
Thobias Andengenye
0 comments:
Post a Comment