Image
Image

MAADHIMISHO YA MIAKA 124 YA SHUJAA ISIKE, LOWASSA ASIMIKWA KUWA CHIFU WA UNYANYEMBE TABORA..



Na.Juma  Kapipi,Tabora.
Maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya miaka 124 ya Shujaa na Mtemi wa Unyanyembe Isike MwanaKiyungi yamefanyika mkoani  Tabora ambapo waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli Bw. Edward  Lowassa alikuwa mgeni rasmi.
 
Katika  maadhimisho  hayo  Bw.Lowassa  alitumia  fursa  hiyo  kuwataka  watanzania  kuona  umuhimu  wa  historia  hiyo  kubwa  ya  Shujaa  huyo  wa  Unyanyembe  aliyethubutu  kupambana  na  udharimu  na  ukandamizaji  dhidi  ya  Waafrika   uliofanywa  na  Wakoloni  pamoja  na  Waarabu  katika  karne  za  17 hadi  20.

Aidha  Bw.Lowassa  pamoja na  kuzungumzia  suala  la  mmomonyoko  wa  maadili  kwa  jamii  na  baadhi  ya viongozi  kwa  ujumla  unaoendelea  kujitokeza  hapa  nchini,aliwataka  wananchi  kuiga  mfano  wa  Shujaa  huyo  wa  Unyanyembe  Isike  MwanaKiyungi  ambaye  alikuwa  mzalendo  na  kuwa  tayari  kufa  kwa ajili  ya  nchi  yake.

Katika  sherehe  hizo  za  miaka  124  Bw.Lowassa  alipata  Baraka  za  kutambikiwa  na  machief  mbalimbali  waliongozwa  na  Mtemi  wa  sasa  wa  Unyanyembe  Chief  Msagati  Ngulyati  Saidi  Fundikira  na  baadae  kuweka  jiwe  la  msingi  katika  eneo  la  Ujenzi  wa  mnara  wa  ngome  ya  Mtemi  Isike  MwanaKiyungi.
Hata  hivyo  baadhi  ya  machief  kutoka  mikoa  ya  Tabora,Katavi  na  Mbeya  kupitia  kumbukumbu  hiyo  wameishauri  Serikali  kuangalia  uwezekano  wa  kutambua  rasmi  uwepo  wa  Machief  hao  hatua  ambayo  itasaidia  kudumisha  maadili  miongoni  mwa  jamii.

Aidha  maadhimisho  hayo  ya  miaka  124  ya Shujaa  wa  Unyanyembe  Isike  MwanaKiyungi  mbali  na  kuhudhuriwa  na  watu  mbalimbali  wakiwemo  viongozi  wa serikali  na  vyama  vya  siasa  pia  yalipambwa  kwa  ngoma  za  asili  ya  kabila  la  wanyamwezi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment