Zoezi la uchukuaji alama za vidole kwa
ajili ya vitambulisho vya Taifa katika wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam
limehitimshwa rasmi leo, huku ikielezwa kuwa wananchi wengi wamejitokeza katika
siku ya mwisho.
Akieleza maendeleo ya zoezi hilo kwa
mbunge wa Temeke Bw. Abbas Mtemvu aliyetembelea mojawapo ya vituo
vinavyoendesha zoezi hilo eneo la Keko, Afisa Usajili wa Wilaya ya Temeke Bw.
Omari Mpangi amesema kwa ujumla zoezi limekwenda vizuri na hakukuwa na matatizo
makubwa.
Bw. Mtemvu ameiomba serikali kuiongezea
uwezo Wakala wa Vitambulisho vya Taifa - NIDA ili ifanikiwe katika azma ya
kuhakikisha watanzania wanapata vitambulisho hivyo vya uraia.
0 comments:
Post a Comment