Wakati huo huo, katibu
mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anatarajiwa kutoa maelezo mbele ya baraza
la usalama la umoja huo baada ya kupotea ripoti ya matokeo ya uchunguzi wa
silaha za kemikali nchini Syria.
Bw Kerry ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na waziri mkuu wa
Israel Bw Benjamin Netanyahu mjini Jerusalem kumweleza kuhusu makubaliano kati
ya Marekani na Russia, na kumhakikisha Bw Netanyahu kuwa rais Bashar al-Assad
amekubali kutoa orodha ya silaha za kemikali za Syria ndani ya wiki moja.
Bw
Netanyahu amesema Syria inatakiwa kunyang'anywa silaha zote za kemikali ili
kuifanya kanda hiyo iwe ya salama.
Mjini Damascus, wakati huohuo, Waziri wa
habari wa Syria Omran al-Zoubi amesisitiza kuwa Syria iko makini katika kuondoa
silaha za kemikali.
Bw Al-Zoubi amesema nchi yake imeanza kuandaa orodha ya
silaha hizo na kuongeza kuwa Syria itatekeleza makubaliano hayo pindi
yatakapoanza kufanya kazi kwa kuheshimu azimio la baraza la usalama.
Bw
Al-Zoubi amesema nchi yake itasaidia kufanikisha kazi wachunguzi wa umoja huo
watakapoingia nchini humo mwezi Novemba mwaka huu.
Akizungumza akiwa nchini
China, Mfalme wa Jordan Abdullah wa pili wa Jordan amesema hofu yao ilikuwa ni
silaha hizo za kemikali kuingia mikononi mwa watu wabaya.
Mfalme Abadullah
amesisitiza kuwa wataongeza juhudi za kufikia makubaliano kati ya umoja wa nchi
za kiarabu na jumuiya ya kimataifa ili kufikia suluhisho la kisiasa katika
mgogoro wa Syria, na hatimaye kumaliza tishio la silaha za kemikali, mapambano
na vurugu nchini Syria.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema ripoti ya
wachunguzi imewekwa kwenye tovuti za idara ya kuteketeza silaha hatari ya umoja
huo.
Wakati huo huo, raia wa Syria wamepongeza makubaliano
yaliyofikiwa kati ya Russia na Marekani. Kiongozi wa kamati ya mambo ya nje ya
bunge la Syria Fadia Deeb, anatoa wito wa suluhisho la kisiasa haraka
iwezekanavyo ili kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
"Hali ya Syria inahitaji suluhisho la kisiasa na pande zote
zinatakiwa kuhimiza utaratibu wa kufikia suluhisho la kisiasa, kwa sababu njia
ya ghasia au ya kijeshi haitasaidia kuleta suluhisho la kisiasa, bali itavuruga
hali ya kanda nzima na maslahi yake.
Katika makubaliano hayo, natumai kuwa
pande zote zimeridhika na hatua hiyo ya usuluhishi".
Waziri wa maridhiano ya
kitaifa wa Syria Bw Ali Haidar amesema makubaliano hayo kama ushindi kwa Syria.
Makubaliano ya kuteketeza silaha za kemikali za Syria pia yanatoa uwezekano wa
kukwamua mazungumzo ya amani kwa ajili ya kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe
nchini humo.
Zaidi ya watu laki 1 wameuawa na wengine milioni mbili kuwa
wakimbizi tangu mgogoro wa huo uanze miaka miwili iliyopita.
0 comments:
Post a Comment