Kwa mara ya kwanza ripoti ya kila mwaka inayohusisha
wahamiaji duniani imeangazia ustawi wa kundi hilo ambapo pamoja na mambo
mengine inaonyesha kwamba kuna kundi kubwa la wahamiaji kutoka nchi zilizoendelea
kwenda zile zinazoendelea huku pia ikiainisha kwamba wale wanaohama kutoka nchi
zilizoendelea kwenda zile zilizoendelea wananufaika zaidi.
Ripoti hiyo
inafuatia utafiti uliofanyika kati ya mwaka 2009 na 2011 uliohusisha nchi 150
duniani na kuratibiwa na shirika la kimataifa la uhamaja IOM.
Pia inaonyesha
kwamba wanaohamia nchi zilizoendelea hawana furaha ukilinganisha na maisha ya
wazawa wa nchi zao licha ya kunufaika kiuchumi.
0 comments:
Post a Comment