Naibu waziri wa Ujenzi
Grayson Lwenge.
Mpango wa ulioanzishwa na serikali wa Matokeo
Makubwa Sasa (BRN) huenda usifanikiwe katika baadhi ya wizara mojawapo ikiwa ni
Wizara ya Ujenzi, ambayo imekumbwa na kashfa ya urasimu wa utoaji wa vibali kwa
baadhi ya kampuni zinazosafirisha mizigo mikubwa, kutokana na watendaji wake
kudaiwa kuendekeza vitendo vya rushwa.
Uchunguzi umebaini kuwa, kutokana na watendaji
wa wizara hiyo kushutumiwa mara kadhaa, Kamati ya Bunge ya Miundombinu
imewataka viongozi wa wizara hiyo kuacha urasimu wa utoaji wa vibali kwani hali
hiyo inaathiri uchumi wa nchi na kuwakimbiza wawekezaji.
Kikao cha kamati ya Bunge na viongozi wa wizara
hiyo kilichoketi Aprili 4 mwaka huu, chini ya Mwenyekiti wake Peter Selukamba,
kilibaini kukithiri kwa urasimu huo na vitendo vinavyoashiria uwapo wa rushwa
kwa watendaji wa wizara hiyo.
Moja ya kampuni ambayo iliwasilisha vielelezo
vyake mbele ya kamati hiyo ikilalamikia urasimu uliopo ndani ya wizara hiyo, ni
pamoja na kampuni ya Usangu Logistics(T) Ltd.
Baadhi ya vielelezo hivyo vinaeleza kuwa
kampuni hiyo ilitekeleza vigezo vya kupata tenda ya kusafirisha mizigo ya
kampuni ya Coca Cola kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Mbeya lakini haikupewa
kibali hadi sasa.
Matokeo yake ilipewa kampuni ya nyingine ambayo
inadaiwa haikufauata taratibu za kisheria ambazo zinataka kampuni ifanye
‘’Rooting Suvey’’ katika barabara husika na kutangaza kwenye vyombo vya habari
kwa siku saba.
Kampuni hiyo inadaiwa kuomba tenda hiyo Januari
21,2010 na kupewa kibali siku iliyofuata Januari 22, 2010 kilichokuwa na namba
BA 27/505/01/E/656.
Kampuni ya Usangu ilisema kuwa, mbali na suala
hilo la upendeleo wa utoaji wa vibali, ilisema kuwa mpaka sasa kampuni hiyo na
zingine hazipewi vibali kwa visingizio kadhaa ili hali watendaji wa wizara
wakiwa moja wa wasaliti wakubwa wa serikali na mawaziri wao.
Mkurugenzi wa kampuni ya Usangu Logistics,
Ibrahim Ismail, alithibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa hadi sasa wizara
imekuwa ikishirikiana na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) kuihujumu
kampuni hiyo na tayari kuna madai yalipelekwa mahakamani na serikali imeshindwa
na inatakiwa kuilipa kampuni hiyo zaidi ya Sh.milioni 48.
Naibu waziri wa Ujenzi Grayson Lwenge,
alipoulizwa, alisema suala la utoaji wa vibali linafanywa na ofisi ya Katibu
Mkuu wa wizara hiyo aliahidi kwama kama kuna tatizo hilo atafuatilia kupata
ukweli kwanini hali hiyo inakuwapo.
Hata hivyo, alisema malalamiko ya
wafanyabiashara hao binafsi hajayapokea na kuwataka wasafirishaji hao
kuyawasilisha wizarani ili yeye na waziri wake waweze kuyafanyia kazi.
Nipashe.
0 comments:
Post a Comment