Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Harrison Mwakyembe akizungumza na wafanyakazi waliogoma wa Mamlaka ya Reli ya
Tanzania na Zambia (Tazara, kwenye stesheni ya Dar es Salaam jana.
Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania na
Zambia (Tazara) wamewasilisha nyaraka nzito kwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harison
Mwakyembe ambazo zinaonyesha jinsi viongozi wa shirika hilo
wanavyojinufaisha kitendo kilichomwacha mdomo wazi waziri huyo kwa mshangao.
Nyaraka
hizo ziliwasilishwa na baadhi ya wafanyakazi zikionyesha jinsi bidhaa zinavyosafirishwa
kutoka Tanzania kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), huku kiasi
kikubwa cha mapato kikibakia mifukoni mwa vigogo wa Tazara.
Katika mkutano
huo, wafanyakazi hao waliwasilisha taarifa za Mkurugenzi mpya wa shirika hilo
kuishi katika hoteli ya New Afrika wakati nyumba anayotakiwa kuishi ikiwa
imepangishwa na mkurugenzi aliyemaliza muda wake kwa kumpangisha mtu mwingine.
Kwa
mujibu wa wafanyakazi hao, waliwasilisha nyaraka zinazotumika kusafirisha
bidhaa kwa kupunguza bei badala ya gaharama halisi inayotakiwa fedha ambazo
huzijulikani zinapokwenda.
Pia wafanyakazi hao walimueleza Dk. Mwakyembe kuwa
Tazara ina madeni makubwa ambayo hayajawahi kuzungumzwa na kuwekwa wazi ili
yaweze kulipwa na badala yake wamekuwa wakisingizia kwamba wafanyakazi wanadai.
Wafanyakazi
hao pia walimueleza waziri huyo kuwa mameneja saba waliokuwa wamefukuzwa
wamerejea kazini na hatua hazijachukuliwa kama ilivyoelekezwa na baraza la
mawaziri kuwa wachunguzwe na kuchukuliwa hatua za kisheria na badala yake wameendelea
kufanyakazi kwa kuharibu vielelezo na nyaraka nyeti.
Mfanyakazi Amiri Husein
alidai kuna mabehewa 26 yalipelekwa DRC lakini fedha zake ziliishia mifukoni
mwa wakubwa.
Alisema Juali 25 mwaka huu, treni iliyokuwa imepakia mafuta
kutoka Tanzania kwenda DRC ambapo zaidi ya Sh. bilioni moja iliyolipwa
iliishia mifukoni mwa wajanja.
Baada ya kupokea taarifa hizo, Dk. Mwakyembe
aliiagiza menejimenti kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma zilizotolewa na
wafanyakazi.
Aliwataka wafanyakazi kurejea kazini leo na wafanyekazi kwa
ueledi na ufanisi mkubwa ili kufidia hasara ya Sh. bilioni 2.4 iliyotokea
wakati wa mgomo.
Waziri huyo alisema Shirika inafanyakazi kwa hasara na
inaelekea kufilisika na kwamba Tanzania na Zambia zimekaa pamoja ili
kulinusuru.
Alisema mapato ya Shirika hilo kwa mwezi ni Sh.bilioni 2.4 wakati
matumizi ni Sh. bilioni 4 na kwamba mambo hayo yanatokana na ufanisi mbovu wa
kiutendaji na kutochukua maamuzi mazito.
0 comments:
Post a Comment