Waziri Mkuu wa Somalia ameahidi kuliangamiza kundi la
kigaidi la al Shabab lililofanya mashambulizi na kuua watu wengi katika jengo
la maduka la Westgate mjini Nairobi, Kenya.
Abdi Farah
Shirdon Saaid amesema wanajeshi zaidi ya elfu 17 wa vikosi vya AMISOM wapo
Somalia na kwamba ana imani kuwa Mogadishu itafanikiwa kuliangamiza kundi la al
Shabab kwa kusaidiwa na wananchi na jamii ya kimataifa.
Waziri Mkuu wa Somalia amesema Somalia na Kenya
zitaendeleza mapambano dhidi ya kundi la al Shabab na kwamba Mogadishu
haitasalimu amri mbele ya matakwa ya kundi hilo kwamba wanajeshi wa Kenya
wanapaswa kuondoka katika ardhi ya Somalia.
Kundi la al Shabab limetangaza kuhusika na shambulio
hilo la Westgate huku likisema kuwa limefanya hivyo kulipiza kisasi kwa hatua
ya Kenya ya kutuma wanajeshi wake huko Somalia.
0 comments:
Post a Comment