Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kumalizika kwa
mzingiro wa jengo la maduka la Westgate huko Nairobi baada ya wafanya
mashambulizi sita kuuliwa na 11 wengine kutiwa nguvuni na vikosi vya usalama
vya nchi hiyo.
Kenyatta amesema mapambano makali ya kuwakomboa mateka
na kuwanasa wafanya mashambulizi huko Westgate yamemalizika na kwamba vikosi
vya usalama vya Kenya vimetoa pigo na kuwafedhehesha wafanya mashambulizi hao.
Amesema raia 61 na wanajeshi sita wameuliwa katika
mkasa huo wa Westgate.
Aidha Rais
Kenyatta ametangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu kuanzia leo
Jumatano.
0 comments:
Post a Comment