Shirikisho la
soka nchini Uingereza linasema kuwa mji wa Instanbul upo katika mstari wa mbele
kuandaa michuano ya nusu fainali na fainali ya mashindano ya barani Ulaya mwaka
2020.
Uingereza ilikuwa na matumaini ya kuandaa michuano
hiyo katika uwanja wa Wembley lakini Katibu Mkuu wa FA Alex Horne anasema mji
wa Istanbul unapigiwa kipaumbele baada ya kukosa nafasi ya kuandaa mashindano
ya Olimpiki mwaka 2020.
Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA linasema kuwa
michuano ya soka ya mwaka 2020 itaandaliwa katika miji 13 katika mataifa 32
ambayo yameomba kuandaa michuano hiyo, na uamuzi utatolewa mwezi Aprili mwaka
ujao.
Awali, rais wa UEFA Michel Platini alisema kuwa
angeunga mkono Uturuki kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ikiwa wangekosa nafasi ya
kaundaa michuano ya Olimpiki mwaka 2020, baad aya Tokyo kupewa nafasi hiyo.
Mbali na Uturuki, Ukraine pia imeomba nafasi ya
kuandaa michuano ya nusu fainali na fainali, huku mataifa mengine 25 ikiwemo
Scotland wameomba nafasi ya kuandaa michuano ya makundi.
0 comments:
Post a Comment