MLEMAVU NCHINI MALAWI AKIWA KAKAA KWENYE KITI.
Tatizo la ulemavu ni kubwa , ikikadiriwa kuwa watu
takribani watu bilioni moja wanaishi na aina Fulani ya ulemavu.
Kila nchi inachagizwa na Umoja wa Mataifa
kuhakikisha mipango yao ya baada ya mwaka 2015 inajumuisha mahitaji na mchango
wa walemavu katika kuleta maendeleo endelevu, kwani bila kuwakwamua walemavu na
maendeleo endelevu itakuwa ni ndoto.
Mataifa mbalimbali sasa yameanza kuchukua hatua za
kuhakikisha ajenda hiyo inapewa kipaumbele na Malawi ni miongoni mwa nchi hizo
kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa viongozi kuhusu ulemavu kwenye Umoja wa
mataifa imewakilishwa na viongozi wa serikali, watu wenye ulemavu na jumuiya
mbalimbali na mashirika yasiyo ya kiserikali kama sight savers na Virginia ni
mwakilishi wake.
"NchiniMalawi
kuna mikakati mingi inayoendelea kuhakikisha watu wenye ulemavu wanajumuishwa
katika sera za maendeleo za taifa , mfano hivi karibuni sheria ya masuala ya
ulemavu imepitishwa ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanajumuishwa
kwenye mikakati ya maendeleo na Sight savers wameshiriki kwa kiasi kikubwa
kugfanya kazi na wajumbe wengine.”
0 comments:
Post a Comment