Wakati mjadala mkuu wa
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukianza leo New York, Marekani ajenda muhimu
ikiwa ni utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia na ajenda ya maendeleo
baada ya mwaka 2015, mwanariadha mashuhuri kutoka Kenya mwenye ulemavu wa macho
Henry Wanyoike amesema hatua zimepigwa kusaidia kundi hilo lakini bado kuna
changamoto.
Mwanariadha Henry wanyoike na msaidizi wakeJoseph Kibunja.
Wanyoike ambaye pia ni balozi mwema wa kamati ya
kimataifa ya michezo ya olimpiki kwa walemavu ametaja mafanikio hususan nchini
mwake akigusia ujumuishi katika michezo.
Kuhusu kuwezesha walemavu kupata huduma mbali mbali
amependekeza kuondolewa ushuru kwa vifaa kama vile vya kusomea au kusikiliza na
hata vya kuwawezesha kutembea.
0 comments:
Post a Comment