Kituo cha televisheni cha Citizen nchini Kenya
kimeripoti kuwa, vikosi vya ulinzi vya Kenya vimewaua wapiganaji sita waliokuwa
bado kwenye jengo la maduka mjini Nairobi.
Awali, serikali
ya Kenya ilisema kuwa kuna wapiganaji kati ya 10 na 15 ndani ya jengo la maduka
ambamo watu 62 wameuawa na wengine 175 kujeruhiwa.
Mapigano mapya yalizuka asubuhi ya leo na kuvunja hali
ya ukimya iliyodumu usiku kucha iliyoashiria kumalizika kwa mapigano kati ya
vikosi vya usalama vya Kenya na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab.
Ofisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka kutaja jina mara
moja amesema, vikosi vya usalama vinafanya msako katika jengo hilo ili
kuhakikisha kuwa hakuna maguruneti au vifaa vyovyote vya kulipuka ambavyo
vimeachwa na magaidi hao.
Ameongeza kuwa, watu hawataruhusiwa kuingia ndani ya
jengo hilo kwa muda kwa kuwa bado kuna miili ya watu ndani ya jengo hilo ambayo
haijatolewa.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anatarajiwa kulihubiria
taifa baadaye leo.
Kundi la Al Shabaab la Somalia limekiri kuhusika na
shambulizi hilo na kusema, limefanya hivyo ili kulipiza kisasi kutokana na
hatua ya serikali ya Kenya kupeleka jeshi lake kusini mwa Somalia kupambana na
wapiganaji wa kundi hilo.
Shambulizi hilo ni kubwa zaidi kutokea nchini humo
baada ya lile la mwaka 1998 ambapo ubalozi wa Marekani nchini Kenya
ulishambuliwa na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab la Somalia na kusababisha
vifo vya watu zaidi ya 200.
0 comments:
Post a Comment