Kiwango cha maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi
kimepungua kwa theluthi moja katika muongo mmoja uliopita kutokana na
kuongezeka kwa fedha zinazotengwa kwa ajili ya matibabu na kupatikana kwa dawa
zenye ufanisi.
Ripoti iliyotolewa na shirika la kimataifa ya
kupambana na Ukimwi UNAIDS inasema mwaka 2012 kulikuwa na maambukizi mapya
milioni 2.3, idadi ambayo imepungua kwa asilimia 33 kuliko mwaka 2011.
Tathmini hiyo pia inasema hadi kufikia mwaka 2012 watu
milioni 9.7 katika nchi zenye mapato ya chini na ya kati waliweza kupata dawa
za ARV, likiwa ni ongezeko la asilimia 20 kwa mwaka mmoja.
Hata hivyo tathmini hiyo inasema kutokuwepo kwa usawa
wa kijinsia, udhaifu kwenye sheria na ubaguzi vinaendelea kukwamisha juhudi za
mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi.
0 comments:
Post a Comment