Msemaji wa Jeshi la
Uganda amesema ulinzi na usalama kwenye mipaka nchi hiyo umeimarishwa.
Uganda kama ilivyokuwa
Kenya ambayo imetuma vikosi vyake nchini Somalia kupambana na wanamgambo wa al
Shabab, imeingiwa na wasiwasi wa uwezekano wa kutokea shambulio kama hilo
nchini humo.
Kundi la al Shabab
lilitangaza kuhusika na shambulio hilo ikiwa ni jibu kwa serikali ya Kenya
ambayo ilituma wanajeshi wake nchini Somalia.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, kundi la al Shabab
liliwahi kutekeleza shambulio la kigaidi na kuwaua watu 77 katika jiji la
Kampala waliokuwa wakiangalia fainali za soka za kombe la dunia mwaka 2010,
zilizofanyika nchini Afrika Kusini.
Paddy Ankunda ameongeza
kuwa, jeshi la Uganda limeimarisha ulinzi na usalama kwenye mipaka ya nchi hiyo
kufuatia shambulio la wanamgambo wa kundi la kigaidi la al Shabab
linalofungamana na mtandao wa al Qaeda ambao wamewaua, kuwajeruhi na kuwateka
nyara watu kadhaa waliokuwa kwenye jumba la kibiashara la Westgate jijini
Nairobi, nchini Kenya.
0 comments:
Post a Comment