Kamanda wa Polisi wa
Nairobi ametangaza kukombolewa idadi ya watu kadhaa waliokuwa wakishikiliwa
mateka na wanamgambo wa al Shabab ndani ya jumba la kibiashara la Westgate
lililoko kwenye mtaa wa Westland jijini Nairobi nchini Kenya.
David Kimaiyo amesema
kuwa, kikosi cha usalama cha Kenya kimefanikiwa kutekeleza operesheni hiyo ya
kuwaokoa baadhi ya watu waliokuwa wakishikiliwa na wanamgambo wa al Shabab na
kusisitiza kwamba operesheni hiyo ya uokozi inaendelea kwa kasi kikubwa.
Wakati huohuo, Polisi
ya Kenya imeeleza kwamba inadhibiti ghorofa zote za jengo la kituo hicho cha
biashara.
Taarifa hiyo imeeleza
kuwa, baada ya masaa machache itafanyika operesheni ya kumaliza kabisa tukio
hilo lililodumu kwa siku tatu. Hadi sasa inaelezwa kuwa, watu wasiopungua 69
wameuawa na wengine wasiopungua 200 kujeruhiwa.
0 comments:
Post a Comment