Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili kuhusiana na suala hilo umebaini kuwa hali hiyo
inasababishwa na mambo mbalimbali, yakiwemo ya kurithi, utumiaji mbaya wa
vyakula na matumizi holela ya vipodozi.
Daktari Adam
Nyalandu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), aliliambia gazeti hili jana
kuwa tatizo la wanawake kuota ndevu linatokana na sababu nyingi ikiwemo
matumizi ya vipozi vyenye kemikali na vyakula vya kusindika.
Alisema
matumizi ya vipodozi vya aina tofauti vyenye viambata vya sumu vimekuwa
vikichangia madhara mbalimbali kwa wanawake ikiwemo uotaji ndevu.
Pia alisema
baadhi ya wanawake wamekuwa wakitumia vipodozi vya aina tofauti ili kutakatisha
ngozi zao zionekane kama za wazungu bila kujua madhara yake. Alisema vipodozi
vingi vina viambata vyenye sumu ambayo ni tishio kiafya.
Dk. Nyalandu
alifafanua kuwa baadhi ya vyakula vya kusindika vimekuwa vikitengenezwa kwa
kutumia kemikali nyingi ambazo zinachangia tatizo hilo kwa wanawake, ambapo
madhara yake kwao yameanza kuonekana wazi wazi.
“Mfano ulikuwa
huli nyama za kopo au vyakula vya kusindika ambavyo kemikali inatumika
kuvisindika sasa unakula, vinaweza kusababisha hilo tatizo hilo kwa kiwango
kikubwa,” alisema Dk. Nyalandu.
Alisema ni vema
wanawake wakawa makini na vipodozi wanavyotumia kwa kuchunguza viatamba vya
sumu ili kuepuka kuvitumia kwa usalama wa afya zao. Kwa upande wake, Dk.
Abdallah Mandai aliwaonya wanawake na kuwataka kuachana na matumizi ya vipodozi
vyenye kemikali sanjari na ulaji wa vyakula vya kizungu.
Alisema
wanawake wengi hususan wa mijini wamekuwa wakitumia vipodozi vyenye kemikali
huku wakila vyakula vinavyoandaliwa kisasa zaidi vikiwa na mafuta mengi au
kukaangwa na hivyo kuharibu homoni zao na kusababisha madhara mbalimbali.
Dk. Mandai
alisema matumizi ya vipodozi si tu yana athari ya kuwafanya wanawake waote
ndevu, bali wengi wao wanapopata ujauzito hujifungua kwa njia ya upasuaji.
“Dawa ya nywele
wanayotumia pamoja na vipodozi vyenye kemikali huchangia kwa kiasi kikubwa
kuota ndevu, katika hili la vipodozi tambua kuwa chochote kinachokuwa juu ya
ngozi ya binadamu kina uwezo wa kusambaa mwilini na kusababisha madhara
mbalimbali,” alisema Dk. Mandai. Akitolea mfano,
alisema zamani
wanawake wakiwemo wajawazito walikuwa wanakula vyakula vya asili na kwamba
walizuiwa hata kula mayai hali iliyokuwa ikiwasaidia wengi wao kujifungua kwa
njia ya kawaida.
“Kuna wakati
wajawazito 10 wanakuwa wamelazwa hospitali, kati yao pengine wawili tu ndiyo
wanaweza kujifungua kwa njia ya kawaida… wengine wanafanyiwa upasuaji,”
alisema.
Aliongeza kuwa
tatizo hilo linaweza kupungua kwa kiasi kikubwa iwapo wanawake watabadilika na
kupenda vitu vya asili na kuacha kuiga utamaduni wa kimagharibi ambao una
athari kubwa kwao.
“Ushauri wangu
ni kwamba tuache kupeperusha bendera ya umagharibi (kuiga tamaduni za kigeni),
tudumishe mila zetu ikiwemo kula vyakula vya asili, matatizo haya yatapungua
kwa kiasi kikubwa,” alisema Dk. Mandai.
Ofisa Uhusiano
wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza alinukuliwa wakati
mmoja akisema mamlaka hiyo imepiga marufuku vipodozi vyote vyenye viambata
sumu, lakini watu wanaendelea kuvitumia.
“Madhara yake
ni makubwa, mwanamke mjamzito ni rahisi kuzaa mtoto taahira, au mimba ikatoka,”
alisema huku Daktari wa Magonjwa ya Ngozi wa Kituo cha Afya Centre, Isaack Maro
akisema wanawake wanaotumia vipodozi vyenye viambata sumu huathirika kwa kiasi
kikubwa bila kujijua.
Alisema madini
ya zebaki yanayotumika katika vipodozi vingi hayatoki kwa urahisi mwilini kwani
hujazana mwilini kwa muda mrefu na kusababisha maradhi.
“Watu
wanaotumia vipodozi hivyo figo zao huwa zimetoboka kutokana na kuharibiwa na
madini hayo,” alisema Dk. Maro.
Source Jmbo leo.
0 comments:
Post a Comment