Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya
Juu Asangye Bangu akiongea na waandishi wa habari Wakati wa kutangaza kuanza
kutumika kwa Huduma ya M-pesa kukusanyia marejesho ya mikopo kwa wanufaika wa
bodi hiyo. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na
Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi Juma Chagonja.
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imetangaza
kuanza kutumia huduma ya M-pesa katika kukusanya marejesho ya mikopo kutoka
kwa wanufaika hatua ikiwa ni katika mikakati ya bodi ya kuimarisha makusanyo ya
urejeshaji wa mikopo hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi Bw. Asangye
Bangu wakati wa zuinduzi wa huduma hiyo mpya
jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa bodi inaendela kujipanga ili kuhakikisha inaboresha
njia za urejeshaji mikopo ili kuwapatia walengwa urahisi.
Mojawapo ya kazi za Bodi ni kusimamia utoaji wa mikopo kwa
wanafunzi waliodahiliwa kwenye vyuo vya elimu ya juu pamoja na urejeshwaji wa
mikopo iliyotolewa na Serikali kwa waliokuwa wanafunzi wa elimu ya juu kuanzia
mwaka 1994 mpaka sasa kwa nia ya kuufanya mfuko wa Elimu ya Juu kuwa endelevu.
"Tunayofuraha kubwa sana leo kutangaza kwamba sasa wanufaika wa
mikopo ya Bodi wanauwezo wa kutumia mfumo wa M-pesa kufanya marejesho ya mikopo
yao moja kwa moja kwa Bodi.
"Alisema Bangu
Bingu amesema bodi
inaimani kuwa M-pesa itawapatia urahisi wanufaika kuweza kutimiza wajibu wao
kisheria wa kurudisha mikopo waliopatiwa kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu.
Ameeleza kuwa wanufaika wa mikopo wanapaswa kuanza kurejesha mikopo yao mara
baada ya miezi 12 kuanzia wanapohitimu masomo ya elimu ya juu au wanapositisha
masomo kwa sababu yoyote ile, akiwa ameajiriwa ama hajaajiriwa.
Amesema kwa upande wa wnufaika walioajiriwa wanalipa mikopo yao kupitia kwa
waajiri wao ambapo hukatwa marejesho ya mikopo kwenye mishahara yao ya kila
mwezi na mwajiri huwasilisha makato hayo kwenye Bodi kupitia kwenye akaunti
zake huku wale ambao sio waajiriwa hupeleka kuwasilisha marejesho ya mikopo
katika benki za bodi.
"Wanufaika wanaorejesha mikopo yao kwa
pesa taslim wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali wakati wa urejeshwaji wa
mikopo yao kupitia kwenye akaunti za Benki ikiwa ni na benki hizo kutokuwa na
matawi ya kutosha yaliyokaribu na warejeshaji wa mikopo pamoja na kutumia muda
mwingi kwenye foleni.
"Alisema , M-pesa itapunguza changamoto hizo na hatimae kuwajengea mazingira
mazuri ya urejeshwaji wa mikopo, Bodi inatangaza rasmi kuanza kutumika kwa
utaratibu huu mpya wa urejeshaji kwa M-pesa kuanzia sasa."
"Alisema Bingu
"
0 comments:
Post a Comment