Mkurugenzi wa Kanda wa
Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann (kulia)
akikabidhi moja ya taa ya Umeme Jua kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi
Dihimba mkoani Mtwara. Anayeshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Nchi ofisi ya
Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (Tamisemi) Mh. Hawa Ghasia
(katikati).
Hoteli ya Double Tree by Hilton ya jijini Dar es Salaam
imeendelea na kampeni zake kabambe ya matumizi ya nishati ya jua kwa kugawa taa
200 kwenye shule ya Msingi Dihimba kata ya Dihimba wilaya ya Mtwara vijijini
Mkoani wa Mtwara.
Akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ya
kugawa taa hizo, Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa na
Tawala za Mikoa (Tamisemi) Hawa Ghasia amesema kwamba msaada huo wa Double Tree
kwa shule hiyo ni kielelezo tosha kwamba sekta binafsi zina mchango mkubwa
katika sekta ya elimu hapa nchini.
“Napenda kuchukua fursa hii adhimu
kuwashukuru uongozi na wafanyakazi wote wa Double Tree kwa msaada wao mkubwa
kwa shule yetu ya hapa Dihimba ambapo watoto wetu watasoma katika mazingira
rafiki yatayowawezesha kufaulu mitihani yao,’ amesema Ghasia.
Waziri Ghasia
amesema kwamba kutokana na mabadiliko ya tabia nchi Serikali, wananchi na wadau
wote wa maendeleo hawawezi kuendelea kutegemea umeme wa vyanzo vya maji na
badala yake umeme wa jua ambao ni nishati mbadala ni ufumbuzi wa tatizo la
nishati nchini.
Amesema mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi hasa
kwenye nishati ni muhimu kwa sababu ni nishati ndio injini ya Uchumi wa taifa
lolote lile hapa duniani kwa sasa.
‘lakini kampeni hizi zitakuwa msaada mkubwa
kwa wanafunzi kutambua na kuelewa nishati mbadala na umuhimu wake katika maisha
ya kila siku ikiwemo mazingira,” alisisitiza
Hoteli ya DoubleTree ilizindua
rasmi kampeni ya matumizi ya nishati ya jua ambayo itadumu kwa muda wa miaka
miwili katika shule za msingi nchi nzima miezi kadhaa iliyopita.
DoubleTree
itakuwa ikigawa taa 200 za mezani zenye kutumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa
darasa la saba kwa shule tofauti kila mwezi, lengo likiwa nikuwafanya wawe na
ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira
kwa kupitia mafunzo katika madarasa yao.
Katika kata ya Dihimba ina jumla ya
wanafunzi wa shule za msingi wavulana 654 na wasichana 645 jumla yao ni 1299.
Shule ya msingi Dihimba imepata mafanikio ya kielimu kwa mwaka 2012/2013 kwa
kushika nafasi ya nne kati ya kata 28 katika mtihani wa taifa wa darasa la saba
mwaka jana.
Katika matokeo hayo shule ya msingi Dihimba ilishika nafasi ya nne
kati ya shule 98 kiwilaya na mafanikio mengine ni kuandikisha wavulana 135 na
wasichana 126 katika kujiunga na darasa la kwanza mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment