MKOA wa Morogoro na vitongoji vyake kwa sasa umegubikwa na
simanzi kubwa baada ya watu watano wa familia moja kufariki kwa mpigo katika
ajali ya gari.
Ajali hiyo iliyohusisha gari ndogo aina ya Toyota Cardina,
yenye namba za usajili T 180 AWT na Fuso namba T324 AWL lililokuwa likiendeshwa
na John Mombozi likitokea Dar es Salaam, ilitokea Oktoba 13, 2013, eneo la
Visiga, Kibaha mkoani Pwani.
NI MHADHIRI WA SUA
Watu waliofariki katika
ajali hiyo ni pamoja na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) aitwaye
Mwaitulo Suma Andalwisye aliyekuwa dereva wa gari ndogo na wanawe watatu;
Gamalieli Mwakyami, Happiness Mwakyami na Jeremy Mwakyani pamoja na mtumishi
wao wa ndani, Elita Mpagama.
Simanzi imeivaa familia hiyo ambayo kwa sasa
imebaki na baba tu aitwaye Jimmy Wilson Mwakyami, mwajiriwa wa Kiwanda cha
Sukari Kilombero, Morogoro ambaye ni Injinia.
IDD YA BALAA
Habari
zilizopatikana eneo la msiba zinasema kwamba, Bi. Mwaitulo (36) alikuwa
akielekea jijini Dar es Salaam ambapo angeiacha familia yake nyumbani kwa mama
yake mdogo, Sister Mwakatogo ili wale Sikukuu ya Idd wakati yeye akiwa safarini
Kampala, Uganda kikazi.
Ilielezwa kuwa, kwa sababu mumewe alikuwa kazini
Kilombero, walikubaliana aichukue familia hadi Dar kwa bibi yao ili aiche hapo
halafu yeye aendelee na safari yake ya Uganda.
“Huyu dada jamani ananiuma
sana...unajua alipata safari ya kikazi kwenda Kampala, sasa akaona si busara
kuwaacha watoto peke yao nyumbani, baada ya kushauriana na mumewe ndiyo akaamua
kuwachukua akawaache kwa bibi yao, akirudi awapitie - kumbe Mungu alishapanga
yake.
“Inauma sana. Mimi namuonea huruma zaidi huyo mumewe. Inahuzunisha sana.
Kuondokewa na familia nzima siyo jambo dogo. Mungu atamwekea wepesi na kumpa
moyo wa ustahimilivu,” alisema jirani mmoja kwa sharti la kutoandikwa jina lake
gazetini kwa kuwa si msemaji wa familia.
SIMULIZI YA MAJONZI
Kati
ya mambo yaliyozidisha majonzi katika ibada ya kuwaombea marehemu hao, Oktoba
15, mwaka huu nyumbani kwao, Sua mjini hapa ni namna ndoto za watoto
waliofariki pamoja na mama yao zilivyozimika kama mshumaa kwenye upepo mkali.
Mtoto
wa kwanza katika familia hiyo, Gamalieli (8) alikuwa anasoma darasa la nne
katika Shule ya St. Marry’s mjini hapa, Happiness (5) alikuwa chekechea na
Jimmy akiwa na umri wa miaka miwili tu wakati mtumishi wao wa ndani akiwa na
miaka 18.
KIU YA ELIMU
Mhadhiri huyo alikuwa mama bora wa kuigwa
katika familia za Kitanzania kwa kuwa alikuwa akipigania sana elimu.
Kabla
hajaanza kazi chuoni hapo, alipata elimu yake hapohapo, pia hadi mauti
yanamkuta alikuwa akiendelea kusoma.
Mwaka 1999 alijiunga chuoni hapo
akitokea Shule ya Sekondari Loleza, Mbeya ambapo alihitimu Shahada ya Kwanza
katika Kilimo cha Bustani ‘Bachelor of Science in Horticulture’ mwaka 2003 na
kuajiriwa hapohapo kama Mhadhiri Mkufunzi.
Katika kujiendeleza zaidi
mwaka 2007 alianza masomo ya Shahada ya Uzamili katika Mimea na Vipando ‘Master
of Science in Crop Science’ ambapo alihitimu mwaka 2009 – akapandishwa cheo na
kuwa Mhadhiri kamili.
Mpaka mauti yanamkuta alikuwa akisaka Shahada ya Uzamivu
‘Doctor of Philosophy – PhD’ chuoni hapo.
BABA ASHINDWA KUZUNGUMZA
FICHUO
TZ imeshuhudia mume wa marehemu Mwaitulo, Jimmy (mwenye shati ya michirizi)
ambaye ajitihadi kujikaza na kupita mbele ya majeneza yote huku machozi
yakimbubujika.
Ijumaa lilitaka kuzungumza naye mawili matatu kuhusiana na
namna alivyoupokea msiba huo, lakini hakuweza kutokana na kuzidiwa na huzuni.
SAFARI
YA MBEYA
Kaimu Mkuu wa SUA, Utawala na Fedha, Profesa Jayro Matovelo
alisema chuo kimepokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa na kwamba marehemu alikuwa
mchakapazi sana.
Baada ya ibada na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu
hao, msafara wa kuelekea nyumbani kwao, Kyela, Mbeya ulianza mishale ya saa 9
alasiri.
0 comments:
Post a Comment