Mwakilishi wa Shirika la Hans Sedel Kanda ya
Afrika Mashariki Konrad Teichert akizungumza katika hafla fupi ya Makabidhiano
ya nakala 10600 za vitabu vya Haki na ulinzi wa mtoto, Fahamu misingi ya amani
na usalama katika familia pamoja na stika 4000 za kupambana na rushwa.Kulia ni
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja pamoja na
Mkuu wa huduma za Polisi Jamii Naibu Kamishna Michael Kamhanda. (Picha na Frank
Geofray-Jeshi la Polisi)
.
Naibu Mwakilishi wa
Shirika la Hans Sedel Kanda ya Afrika Mashariki Konrad akimkabidhi moja ya
stika za kupamba na rushwa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa
Jeshi la Polisi Paul Chagonja wakati wa hafla fupi ya Makabidhiano ya nakala
10600 za vitabu vya Haki na ulinzi wa mtoto, Fahamu misingi ya amani na usalama
katika familia pamoja na stika 4000 za kupambana na rushwa zilizochapishwa na
shirika hilo.Kulia ni Mkuu wa huduma za Polisi Jamii Naibu Kamishna Michael
Kamhanda.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Naibu Mwakilishi wa
Shirika la Hans Sedel Kanda ya Afrika Mashariki Konrad akimkabidhi moja ya
kitabu cha Haki na ulinzi wa mtoto Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa
Jeshi la Polisi Paul Chagonja wakati wa hafla fupi ya Makabidhiano ya nakala
10600 za vitabu vya Haki na ulinzi wa mtoto, Fahamu misingi ya amani na usalama
katika familia pamoja na stika 4000 za kupambana na rushwa zilizochapishwa na
shirika hilo kwa lengo la kulisaidia jeshi la Polisi katika kupambana na
uhalifu jijini Dar es Salaam jana.Kulia ni Mkuu wa huduma za Polisi Jamii Naibu
Kamishna Michael Kamhanda. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
.
..................................................................................................................................................................
Na Tamimu Adam.
Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi
limekabidhiwa zaidi ya nakala 10600 za vitabu vya Polisi jamii
na ulinzi shirikishi kutoka shirika la Hans Sidel
Foundation ambavyo vitatumika katika kuendelea kuhamasisha
dhana ya Polisi jamii na ulinzi shirikishi pamoja na kuendeleza mpango wa
kufikisha elimu ya usalama hadi ngazi ya familia.
Nakala za vitabu zilizokabidhiwa
ni kitabu cha Haki na Ulinzi wa mtoto, nakla 5300 na kitabu cha
fahamu misingi ya amani na usalama katika familia nakala 5300 pamoja
na stika 4000 za kupambana na rushwa.
Vitabu hivyo vilikabidhiwa na Mwakilishi wa shirika la Hans Sidel
Bw. Konrad Teichert na kupokelewa na Kamishina wa Opereheni na
Mafunzo (CP) Paul Chagonja kwa niaba ya Jeshi la Polisi katika hafla fupi
iliyofanyika jana Makao makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es salaam.
Chagonja alisema kuwa vitabu hivyo vimefika
wakati muafaka ambapo Jeshi la Polisi linaendelea na mpango wake wa kufikisha
elimu ya usalama hadi ngazi ya familia pamoja na mapambano dhidi ya rushwa
ambayo kila mmoja anatakiwa kuwajibika ili kutokomeza rushwa hapa nchini.
Aliongeza kuwa vitabu
hivyo vinalenga katika kuimarisha ulinzi shirikishi na
kuwawezesha kila mmoja katika familia kuwezeshwa na kujengewa uwezo
katika kubaini na kuzuia fursa za kutendeka kwa uhalifu au vurugu ndani ya
jamii.
Kwa upande wake
Mwakilishi wa shirika la Hans Sidel Bw. Konrad Teichert alisema wataendelea
kushirikiana na jeshi la Polisi katika kusaidia kufanikisha maboresho ya jeshi
hilo pamoja na kuendelea kufanya mafunzo ya kuwajengea uwezo Maofisa na Askari
wa Jeshi la Polisi.
Naye Mkuu
wa Ufuatiliaji na tathimini wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishina wa Polisi,
(DCP) Omar Rashid alishukuru shirika la Hans Sidel kwa ushirikiano walioutoa
katika kusaidia kuchapisha vitabu hivyo na kuendesha mafunzo ya kuwajengea
uwezo , maofisa, wakaguzi na askari, ambapo jumla ya wahitimu 17 walitunukiwa
vyeti vya mafuzo hayo.
0 comments:
Post a Comment