SIKU moja
baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki kumtuhumu Mkuu
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Arusha (RCO), Dawal Nyenda, kusaidia
majangili kutoroka nje ya nchi, jeshi la polisi limech
ukua hatua ya kuunda
timu kuchunguza tukio hilo.
Wakati hayo yakijiri, RCO Nyenda
amesema yote yanayotokea anamuachia Mungu, na kwamba hawezi kusema chochote kwa
sababu anamheshimu Kagasheki kama mkuu wake wa kazi.
Akizungumza na NIPASHE Jumapili,
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Advera
Senso, alisema Mkuu wa jeshi hilo nchini, (IGP) Said Mwema, ameteua timu maalum
ya watu watakaokwenda jijini Arusha kuchunguza ili kupata ukweli.
Alisema baada ya kupata taarifa
hizo, walipata mshtuko kitu ambacho kilimfanya IGP Mwema kuchukua hatua hiyo na
kuahidi matokeo ya uchunguzi huo yatawekwa wazi ili kila mwananchi afahamu.
"Jeshi la polisi linafanya
kazi kwa sheria na utaratibu, inapotokea mtumishi hasa kiongozi wa juu
kutuhumiwa, hatua mbalimbali zinachukuliwa ikiwamo kufanya uchunguzi kwa mujibu
wa sheria," alisema Senso.
Hata hivyo, Senso hakuwa tayari
kutaja timu hiyo ina watu wangapi na itachukua muda gani kukamilisha kazi,
badala yake alisema wananchi wanatakiwa kuliamini jeshi lao na majibu
yatapatikana haraka.
"Unajua kazi za jeshi ni
vigumu kukupa taarifa za kila kitu kinachofanyika, kitu muhimu hapa ni kwamba
polisi imeshtushwa na jambo hili na kazi hiyo itafanyika kwa uwazi mkubwa,"
aliongeza kusema.
Alisema timu hiyo itafanya kazi
ya msingi ya kusikiliza kila upande na endapo ikibainika kuna ukweli, taratibu
za kijeshi zitachukuliwa.
RCO 'NAMUACHIA MUNGU'
Akizungumza kwa njia ya simu
kutoka mkoani Arusha, RCO Nyenda alisema mpaka sasa hajui kosa lake, hivyo yote
anamuachia Mungu ndiye anayejua ukweli wa jambo hilo.
Alisema yeye hajui chochote juu
ya tuhuma hizo kwani waziri hakumlalamikia wala kumtaarifu kama kuna jambo
limemkera yeye amelifanya.
"Mimi sijui chochote, taarifa
zote nimezisoma kwenye magazeti na kusikia kupitia runinga, muulizeni Kamanda
wa Mkoa kama yeye aliambiwa jambo hilo," alisema Nyenda.
Hata hivyo, alisema hawezi
kujibizana na kiongozi huyo kwa sababu anamheshimu kama mkuu wake wa kazi.
WAZIRI NCHIMBI: "NIPO
NJE"
Alipotafutwa Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi kuzungumzia sakata hilo, alisema kupitia
simu yake ya mkononi kwamba hana taarifa kwa sababu yupo nje ya nchi kikazi.
"Ndugu mwandishi habari hii
kwangu ni mpya, nakuomba wasiliana na mtu niliyemuachia ofisi kwani kwa sasa
nipo nje ya nchi," alisema.
Juzi wakati akitangaza uwapo wa
`operesheni tokomeza majangili' nchini kote, Waziri Kagasheki alimtuhumu RCO
huyo wa Arusha kushiriki katika mchakato wa kuwatorosha raia wawili wa Saud
Arabia ambao walituhumiwa kwa ujangili.
Alisema, watu walikamatwa wakiwa
na silaha na baadhi ya vithibitisho vinavyoonyesha walikuwa wakifanya kazi
hiyo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPIL
0 comments:
Post a Comment