Uwezekano wa mtu mmoja aliyetumia dawa za kulevya kutolewa damu
yake kidogo na kutumiwa na watu wengine wawili na kulewa kwa kiwango kilekile,
utatolewa ufafanuzi wa kisayansi toleo lijalo. Picha na Maktaba.
“Kitengo chetu kilianza kutoa huduma hii Februari 2011 na tulianza
kupokea wagonjwa wanne kwa siku na ilifikia hatua tulikuwa tukipokea hata 20
waliohitaji huduma kutoka kwetu na mpaka sasa tuna wagonjwa 640.
Kati ya hawa 18 tuliwaondoa kutokana na matatizo mbalimbali. Wapo
waliokuwa wakifika na silaha mbalimbali na hawa walikuwa tishio kwa kitengo
hiki.”
Dk Masao anasema licha ya kuondolewa katika kitengo hicho walio wengi
wamekuwa wakirudishwa tena;
“Hata kama akifanya vurugu tutamwondoa lakini baadaye lazima tumfuate na
kama akikiri kosa na kuahidi kubadilika tunamrudisha na anaendelea na dozi.
Kila anayetibiwa hapa sharti la kwanza ni lazima makazi yake halisi yajulikane
hivyo inakuwa rahisi kumfuatilia mgonjwa huyu iwapo atakatisha dozi ili kujua
sababu ni nini.”
Akifafanua kuhusu dawa inayotumika kuondoa sumu ya dawa za kulevya
katika mwili wa mwathirika, Dk Masau alisema methadone humwezesha mgonjwa
kutosikia hamu ya kutumia dawa hizo, sambamba na kumwondolea maumivu mwilini.
“Dawa hii wanayopewa inawasaidia mwili kutokuwa na maumivu. Maana mtu
anaposikia maumivu hapo ndipo anapoanza kuhangaika kutafuta heroin ili
ajidunge.
Lakini akipata methadone huwa salama na hawezi kupata tena hamu ila
masharti ya dawa hii ukitumia hupaswi kurudi tena na kuanza kujidunga,” alisema
Dk Masau na kuongeza; “Dawa hii yenye thamani ya dola 75,000 sawa na Sh124
milioni tumepewa na wafadhili kutoka Canada ambapo walitoa kiasi cha kilogramu
50 ambazo huweza kutumika kwa kipindi cha miaka miwili.”
Anafafanua kuwa dozi hiyo hutolewa kila siku katika hospitali hiyo kwa
kiasi cha dozi ya mililita 1.5 kwa kila mwathirika kila siku huku wengine
wakitunzwa wodini kutokana na kuathirika kwa kiwango kikubwa, hata hivyo
aliweka wazi kuwa idadi kubwa wamekuwa wakishindwa kuhimili gharama za usafiri
kila siku.
Alisema Tanzania ni nchi ya kwanza katika nchi za Jangwa la Sahara kuwa
na kitengo cha methadone.
“Tanzania ni nchi ya kwanza katika nchi za Jangwa la Sahara kuanza kutoa
matibabu ya methadone, lakini pia tunafundisha nchi nyingi kutoa huduma hii
wakiwemo Nigeria, Msumbiji, Kenya, Uganda, Zambia na nchi nyinginezo ambao
hufika hapa Muhimbili kwa ajili ya kupata utaalamu huu,” alisema Dk Masao.
Alisema utaalamu hasa kuhusu matumizi ya dawa hiyo sambamba na ujuzi wa
kutoa matibabu hayo waliupata katika nchi ya Vietnam.
“Vietnam ndipo hasa tulipopata ujuzi huu na huko tumekuwa tukiwapeleka
wataalamu wengi kujifunza.
Moja kati ya changamoto zilizopo katika kitengo hiki ni ukosefu wa watoa
huduma, wengi hawapo radhi kujitolea katika kutoa matibabu kwenye kitengo hiki.
Hatuna wanasaikolojia wa kutosha, manesi na madaktari”.
Dk Masao anasema kitengo hicho kimekuwa kikipokea pia wanandoa ambao
wamekuwa wakifika kwa pamoja kwa nia ya kupata huduma hiyo ili waachane na
matumizi ya dawa za kulevya.
Kuhusu uwezekano wa mtu mmoja aliyetumia dawa za kulevya kutolewa damu
yake kidogo na kutumiwa na watu wengine wawili na kulewa kwa kiwango kilekile,
utatolewa ufafanuzi wa kisayansi toleo lijalo. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment