Kesi hiyo ilifunguliwa kwa
ushirikiano wa Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Chama
cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
Katika kesi hiyo namba 24 ya
mwaka 2013, LHRC na TLS, wanadai kuwa Pinda alivunja katiba kwa kauli aliyoitoa
Bungeni kuhusu polisi kuwapiga raia wanaokaidi amri.
Walalamikaji hao wanadai kuwa
kauli hiyo ni amri kwa vyombo vya dola kutekeleza sheria ya kuwapiga wananchi,
wakati wa vurugu.
Hata hivyo Pinda na AG katika
majibu yao, wamewasilisha pingamizi la awaliambalo pamoja na mambo mengine
wanadai kuwa walalamikaji na watu waliorodheshwa katika kesi hiyo, hawana
mamlaka kisheria kufungua kesi hiyo.
Pingamizi hilo limepangwa kusikilizwa leo na
jopo la majaji linaloongozwa na Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu.
0 comments:
Post a Comment