Image
Image

BENDERA ACHEFUKA NA WANANCHI WANAOJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA KUHATARISHA AMANI YA NCHI.


Kufuatia baadhi ya wananchi kuamua kujichukulia sheria mikononi hasa pale wanapokuwa wanahitaji kutatuliwa masuala yao ya msingi na watu walio wachagua na kuwaweka madarakani, Hatimaye Mkuu wa mkoa wa morogoro Joel Bendera amesema amekerwa na tabia ya baadhi ya watu hao kwani husababisha  uvunjifu wa amani wa nchi na wengine kupoteza maisha kwa  suala ambalo lingeweza kuzungumzika na kupata suluhisho.

Amesema mambo ambayo hutokea maranyingi katika sehemu mbali mbali za mikoa ya tanzania na hata katika jiji watu hao hujazana ujinga kwenye akili zao na hatimaye kuamua kujichukulia hatua ya  wengine kudiriki kuziba barabara kwa kuweka mawe, magogo na wengine kulala barabarani kwa nia ya kushinikiza  kutatuliwa kero zao za muda mrefu jambo ambalo linachafua taswira ya nchi yetu ya tanzania.


Kauli ya Bendera wakati wa mazungumzo yake na  waandishi wa habari ofisini kwake mkoani morogoro alisema kuwa amelazimika  kutoa kauli hiyo  kwa wananchi baada ya kuona tabia hizo za kuziba barabara kuendelea  kushamiri katika maeneo mengi ya mkoa huo. 



“Ni marufuku kwa mtu ama kikundi katika kijiji au mji wowote kuweka vizuizi barabarani kwa kisingizio cha kupata ufumbuzi wa kero yoyote na atayefanya vitendo hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa hata kushtakiwa na vyombo vya dola,”alisema Bendera.



Hivi karibuni kumezuka tabia ya baadhi ya wananchi katika vijiji kuweka vizuizi kama mawe,magogo na hata wengine kulala barabarani ili kuzuia magari yasipite kwa lengo la kushinikiza kutatuliwa kero zao na viongozi wa ngazi za juu,jambo linalosababisha vurugu na hata kupoteza amani ya nchi. 




Alisema kwamba  tabia ya kuweka vizuizi katika barabara kuu kwa lengo la kushinikiza kiongizi wa ngazi yoyote kutaka atatue kero yake imekuwa ikisababisha madhaara makubwa hasa kwa watumiaji wa barabara yakiwemo magari ya nchi za nje.

“Nakerwa sana na tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi  kwa kujihusisha na uwekaji wa vizuizi barabara kwa kisingizio cha kushinikiza kutatuliwa  kero zao  jambo sio zuri na sasa tayari kamati za ulinzi za wilaya na mkoa nimeziagiza kufatilia suala hili  kwa lengo la  kulikomesha tabia hii,”alisema Bendera.



Hata hivyoBendera aliwataka wananchi kufuata taratibu za kuweza kutatuliwa kero zao  ndani ya vijiji kupitia ngazi stahiki ikiwemo kuonana na uongozi wa ngazi ya kitongoji, kijiji, kata, tarafa, wilaya, hadi kufika mkoa na taifa, kero hizo zitapatiwa ufumbuzi.


Aidha ameongeza kwa kusema kuwa vipo  vijiji ambavyo vimekumbwa na kuwekwa vizuizi barabarani ni wakati inapotokea kadia kama hiyo ni, mji mdogo wa Dumila, Doma,Turiani na Dihombo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment