Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar
Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wananchi kuacha tofauti zao na badala yake
waishi kwa kuvumiliana.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo jana wakati akitoa mkono wa Iddi el-Hajj kwa baadhi ya wazee na mayatima
wa vijiji vya Jumbi, Chwaka na Marumbi katika Wilaya ya Kati Unguja.
Amesema hakuna haja
kwa wanajamii kuendeleza migogoro isiyokuwa ya lazima, kwani haina tija yoyote
kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Katika hatua nyengine
Makamu wa Kwanza wa Rais amewasisitiza wananchi kusherehekea sikuu ya
Eid-el-Hajj kwa njia za amani na kufuata maadili ya Kiislamu pamoja na maadili
ya Zanzibar.
Mapema asubuhi Maalim
Seif alijumuika na viongozi wengine wa kitaifa pamoja na waislamu mbali mbali
katika sala ya Eid iliyosaliwa kitaifa katika viwanja vya Marumbi na baadaye
kujuika katika Baraza la Eid-El-Hajj lililofanyika Chuo Kikuu Cha Taifa cha Zanzibar kilichoko Tunguu.
0 comments:
Post a Comment