Nyota wa sinema za Kibongo, Ummy Wenceslaus maarufu kama 'Dokii' amewashangaa watu wanaomsema kuwa
anajipendekeza kwa Rais Jakaya Kikwete na kuwataka waache propaganda zisizo na tija kwani yeye
hajipendekezi hata kidogo.
Amelazimika kutoa kauli hiyo wakati wa mahojiano yake na Kipindi cha Action & Cut kinachorushwa na kituo cha Channel Ten hivi karibuni, ambapo Dokii alisema kutokana na jinsi alivyoshiriki katika kampeni mbalimbali za Kikwete hadi kupata ajali na kuumia mkono, wambeya wamekuwa wakimzushia kuwa alijipendekeza na hakupewa msaada wowote alipoumia jambo ambalo sio zuri.
“Nawashangaa wanaosema kuwa najipendekeza kwa JK, eti wanasema nilitelekezwa. Kwa taarifa yao tu ni kwamba, JK aliposikia nimepata ajali, alituma madaktari Wazungu kuja kunihudumia.
“Halafu hata wakisema najipendekeza pia naweza nikakubali, nisipojipendekeza kwake wanataka nikajipendekeze kwa nani? Najua hata wao wanatamani kuwa karibu na viongozi kama mimi,” alisema Dokii.

0 comments:
Post a Comment