Simanzi, Vilio na hali ya huzuni
jana vilitawala kwa mamia ya wakazi wa kijiji cha Shari, Machame wilayani Hai
waliojitokeza kuuaga mwili wa marehemu ,Anastazia Saro (56),mama mzazi wa
Mwanadishi na Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV,Ufoo Saro.
Wakazi hao wakiwemo wale waliotoka
maeneo mbalimbali ya miji ya Moshi,Arusha na Dar es Salaam
baadhi yao
walionekana wakiangua vilio huku wengine wakipoteza fahamu muda mfupi baada ya
jeneza lililobeba mwili wa marehemu kuingizwa kanisani.
Hali ilikuwa ya Simanzi zaidi
wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa waombolezaji wakipita mbele ya jeneza
ambapo ililazimika kuwepo na watu maalumu ambao walikuwa na jukumu la kutoa
huduma ya kwanza kwa baadhi ya ndugu walioshindwa kujuzuia.
Hali kama hiyo ili rejea kwa mara
nyingine tena pale msemaji wa familia Allelio Swai akitoa maelezo ya namna
marehemu alivyo uawa na hali aliyokutwa nayo mara baada ya kufanyiwa uchunguzi
na madaktari.
Akitoa maelezo ya wasifu wa
marehemu aliyefanyiwa ibada ya mazishi katika Kanisa la Urara lililopo chini ya
Jimbo la Hai la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Swai alisema
marehemu Anastazia Saro alifikwa na mauti hayo baada ya kupigwa risasi na
mkwewe Anthery Mushi ambaye alikwenda nyumbani kwa mama huyo eneo la Kibamba
CCM,nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Alisema taarifa ya madaktari
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), inaonyesha,Anastazia Saro
alifariki dunia baada ya kushambuliwa kwa risasi tano katika mwili wake.
Swai aliomba kufanyika maombi kwa
ajili ya Ufoo aliyelazwa katika hosptali ya Muhimbili ambako anapatiwa matibabu
baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa hali iliyolazimu madaktari kumpa muda mrefu
wa mapumziko.
“ Ufoo taarifa ya madaktari
inaonesha alichanika utumbo mkubwa na kiasi utumbo mdogo,lakini tunashukuru
hali ya Ufoo inaendelea kuimarika ,lakini maombi yenu yanahitajika ili aweze
kurejea katika hali yake ya zamani ,na aweze kulitumikia taifa kwa kuhabarisha
“alisema Swai.
Kwa upande wake,baba mdogo wa Ufoo
Saro, mzee Eshikaeli Saro, akizungumza katika ibada ya mazishi kanisani
hapo,alisema familia na kanisa imepoteza mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya
jamii na kanisa.
“Mama alikuwa ndiye mpambaji wa
madhabahu ya kanisa ,na alihakikisha kanisa linakuwa katika hali ya usafi kabla
ya ibada na hata pale wanakwaya walipokuwa na mazoezi ya kutwa hapa kanisani
alihakikisha wanapata chakula”alisema Saro.
Alitoa shukrani kwa Mwenyekiti wa
makampuni ya IPP, Dk.Regnald Mengi,mkurugenzi mtendaji wa ITV na Redio One,
Joyce Mhavile pamoja na wafanyakazi wote wa makampuni hayo kwa kuifanya familia
hiyo iweze kumfikisha marehemu Machame na kuzikwa.
Marehemu Anastazia Saro, aliuawa
baada ya mkwewe kufika nyumbani kwake Kibamba CCM akiwa na mzazi mwenzie Ufoo
kwa lengo la kusuluhishwa kile kinachodaiwa ni ugomvi uliokuwa ukifukuta kati
ya wawili hao.
Tukio hilo lilitokea alfajiri ya
Jumapili ya Oktoba 13 mwaka huu, huku mwanae Ufoo Saro ambaye ni Mwandishi na
Mtangazaji wa ITV, akijeruhiwa vibaya kwa risasi mbili baada ya kutokea ugomvi
kati yakena mzazi mwenzie Anthery Mushi ambaye hata hivyo na yeye alijiua kwa
kujipiga risasi baada ya tukio hilo.
Mwenda pole.blogsports,Arusha.
0 comments:
Post a Comment