Mtoto Alvis Anthery akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la
marehemu Bibi yake Anastazia Saro aliyezikwa jana katika makaburi ya kanisa la
Urara wilayani Hai.
Huu ni umati wa waombolezaji waliojitikeza katika kuuaga
mwili wa marehemu Anastazia Saro aliyefariki baada ya kupigwa risasi na mkwewe wiki iliyo pita jijini Dar es Salaam, Ambapo amezikwa katika makaburi ya kanisa la Urara
wilayani Hai.
Huyu ni msemaji wa familia ya Saro,Allelio Swai akionekana akizungumza wakati akitoa
maelezo ya familia wakati wa ibada ya kumuombea marehemu Anastazia Saro huko urara wilayani Hai.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Anastazia Saro
likiwekwa kaburini kwa unyenyekevu wa hali ya juu, ambapo ndio safari ya mwisho kwake, huku nasi tukiwa kwenye foleni .
Hapa baadhi ya watu wakiwa wamelibeba jeneza hilo lenye mwili wa marehemu anastazia saro kwaajili ya kwenda kupumzishwa kwenye nyumba ya milele.
Mkuu wa jimbo la Hai,Aminirabi Swai akiongoza ibada
ya maziko katika makaburi ya kanisa hilo na
kisha kuweka shada la maua
katika kaburi la marehemu Anastazia Saro huko urara wilayani Hai.
Mwakilishi
wa serikali katika maziko ya marehemu Anastazia Saro ,mkuu wa wilaya ya Hai
Novatus Makunga akiweka shada la Maua
katika kaburi hilo.
Mtoto wa mwandishi wa Habari wa ITV/ Radio One Ufoo Saro, Alvis Anthery akiweka shada la maua katika kaburi la Bibi yake marehemu Anastazia
Saro, (Picha na Mwenda Pole na Upole Wake Arusha.
0 comments:
Post a Comment