Serikali ya
Kenya imetuma vikosi maalum vitatu kupambana na hali ya kuongezeka kwa matumizi
ya dawa za kulevya na uwepo wa silaha haramu, vinavyoathiri vijana wasiokuwa na
ajira katika sehemu ya kaskazini mwa Kenya.
Hatua ya serikali hiyo inatokana
na wasiwasi waliouonesha wazee wa kikabila katika sehemu ya kaskazini mwa
Kenya, waliosema matatizo hayo yanachangia kuvuruga usalama katika sehemu ya
kaskazini mwa Kenya.
Katika miezi ya
hivi karibuni kumekuwa na tatizo la kuongezeka kwa uhalifu katika eneo la Bungoma,
ambako watu 30 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, katika eneo la Trans
Nzoia watu 15 waliuawa, ikiwa ni pamoja na polisi watatu.
Watu hao waliuawa na
majambazi walionunua silaha haramu kutoka Uganda.
Tatizo la umasikini na
ukosefu wa ajira yanachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la uhalifu katika
sehemu mbalimbali za Kenya.


0 comments:
Post a Comment