Mechi ya Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Simba na Tanzania Prisons kutoka Mbeya
iliyochezwa jana (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza
sh. 60,521,000.
Simba iliibuka na
ushindi wa bao 1-0 katika mechi hiyo namba 55 na kushuhudiwa na watazamaji
10,494 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na
sh. 20,000.
Kila klabu ilipata
mgawo wa sh. 14,191,002.55 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa
ni sh. 9,232,016.95.
Mgawo mwingine wa
mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,215,763.96, tiketi sh. 3,183,890,
gharama za mechi sh. 4,329,458.37, Kamati ya Ligi sh. 4,329,458.37, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,164,729.19 na Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,683,678.26.
Boniface
Wambura Mgoyo
Ofisa
Habari
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)



0 comments:
Post a Comment