MWANAFUNZI wa shule ya
sekondari ya Idodi iliyopo katika wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa
Lusinde Nyaulingo amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa baada ya kupewa
adhabu ya viboko visivyo na idadi na mwalimu wake na kisha kufungiwa katika
bweni kwa zaidi ya siku 3 ili kuficha uovu huo.
Tukio hili linakuja
wakati ambapo kumekuwa na jitihada kubwa zikifanywa na serikali na asasi
mbalimbali kukemea vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Ni mwanafunzi Lusinde
anayesoma kidato cha tatu anaugulia maumivu makali baada ya kufanyiwana ukatili
uliomsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake kufuatia kutuhumiwa
kuiba simu ya mwanafunzi mwenzake hali inayomfanya kupoteza muda mwingi wa
masomo wakati akiendelea na matibabu.
Lusinde anasema baada
ya kuangushiwa kipigo hicho kikali, kilichodumu kwa zaidi ya masaa tatatu,
alipoteza fahamu na kisha kufungiwa katika bweni kwa siku tatu, huku wanafunzi
wenzie wakipigwa marufuku kufikisha taarifa ya ugonjwa kwa wazazi wa Lusinde.
Kaka wa mwanafunzi
Lusinde anauzungumziaje ukatili huu?
Kwa upande wake muuguzi
katika wodi ya majeraha katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa Bi Beatrice Tilya amethibitisha kumpokea
mwanafunzi huyo.
Hata hivyo jeshi la
polisi kupitia kamanda wake mkoa wa Iringa ACP Athmani Mungi amesema
anafuatilia tukio hilo ili kuhakikisha haki inatendeka, kwa kumchukulia hatua
za kisheria mtuhumiwa ikiwa pamoja na kumfikisha Mahakamani.


0 comments:
Post a Comment