Chama cha mapinduzi CCM
kimewaasa wanachama wake kuwa na maadili mema na kuacha tabia ya sasa ya
kutuhumiana ndani ya chama wao kwa wao.
Hayo yamebainishwa na
Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi wa Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam
Rutami Masumu wakati wa Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika viwanja vya Yombo
Vituka Jijini Dar es Salaam, ukiwa ni Mkutano wa kawaida kwa wananchi na kusoma
taarifa ya utekelezaji ya ilani ya Uchaguzi wa mwaka 2010 uliotolewa na Rais
Jakaya Kikwete.
Amesema wanachama
wanapaswa kukaa kwa ushirikiano na kufanya kazi za kichama kwa pamoja kwani kwa
sasa kuna baadhi ya wanachama wanatumika kukivuruga chama, kitendo ambacho
husababisha kutotekeleza malengo ya chama pamoja na ahadi walizotoa kwa
wananchi wao.
Naye Mbunge wa Jimbo la
Temeke Bw. Abas Mtemvu ameahidi kuendelea kuwasaidia akina mama na vijana
waliojiunga katika mifuko ya
kujiimarisha kiuchumi ikiwemo VIKOBA, ambapo zaidi ya milioni 300 zimetengwa
kwa ajili ya kuwapa mikopo.


0 comments:
Post a Comment