Mkurugenzi wa reli
ya Tanzania na Zambia TAZARA, Bw Ronald Phiri amesema ana matumaini makubwa na
uhakika kwamba reli ya TAZARA itakuwa na mustakbali mzuri hususan kutokana na
vifaa sahihi pamoja na msaada wa kifedha.
Bw Phiri amesema
hayo alipokuwa akizungumza na ujumbe wa maofisa kutoka China ambao upo Tanzania
kukagua miradi iliyodhaminiwa kupitia makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na
kiteknolojia kati ya China na Tanzania.
Ameeleza kuwa
amekutana na wateja wengi pamoja na makampuni ambayo yameeleza nia yao ya
kuacha kutumia usafiri wa barabara na kutumia usafiri wa reli, jambo ambalo
linatoa ishara ya kuwepo kwa soko kubwa kwa reli ya TAZARA.
Kwa upande wake
kiongozi wa ujumbe huo Bibi Chen Rong ambaye pia ni mkurugenzi wa divisheni ya
ofisi ya utendaji ya ushirikiano wa kimataifa na kiuchumi ya wizara ya biashara
ya China, amesema watu wa China wanaithamini TAZARA na kuona ni kama alama
kubwa ya urafiki na ushirikiano kati ya nchi tatu za China, Tanzania na Zambia
na kusisitiza kuwa China siku zote itaisaidia reli ya TAZARA.
0 comments:
Post a Comment