Waziri wa habari
wa Malawi Bw Brown Mpinganjira amesema Rais Joyce Banda wa Malawi ambaye
ametangaza vita dhidi ya ufisadi nchini Malawi amekuwa akitishiwa kuuawa.
Vitisho dhidi ya
Rais Banda vimekuja wakati maofisa wakubwa na wa kati wa Malawi wanaendelea
kukamatwa kutokana na kuhusika na vitendo vya ufisadi.
Mwezi Septemba
mhasibu msaidizi wa wizara ya fedha ya Malawi alikamatwa na zaidi ya dola laki
3 za kimarekani kwenye gari yake na nyingine zikiwa nyumbani kwake.
Mhasibu huyo
alikamatwa baada ya mkurugenzi wa bajeti wa Malawi kujeruhiwa kwa risasi na
watu wasiojulikana, na baadaye kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya
matibabu.
Wakati serikali ya
Malawi ikiendelea na uchunguzi kuhusu jaribio la kuuawa kwa mkurugenzi wa
bajeti, kumekuwa na taarifa nyingi kuhusu kamatakamata ya maofisa wa serikali
wanaohusika na vitendo vya ufisadi katika serikali ya Malawi.
0 comments:
Post a Comment