Baada ya kuwa na
nafasi kuu katika kuharibu miundo mbinu ya Libya, hatimaye Muungano wa kijeshi
wa (Nato) umesema kuwa utatuma timu ya wataalamu ili kuisaidia nchi hiyo ya
Kiarabu kuimarisha taasisi zake za kijeshi na kiulinzi.
Nato imesema kuwa
imeafiki ombi lililotolewa na Ali Zeidan Waziri Mkuu wa Libya la kutoa ushauri
katika suala la kuimarisha taasisi za kiulinzi za nchi hiyo.
Hata hivyo nato
imeongeza kuwa itaunda timu ndogo ya ushauri ya watu wasiozidi kumi kwa ajili
ya kazi hiyo.
Aidha msemaji wa
NATO Carmen Roman amesema timu hiyo haitakuwa na kambi ya kudumu huko Libya na
kwamba itafanya shughuli zake kutokea Ubelgiji.
0 comments:
Post a Comment