Vikosi vya usalama
vya Misri vimelazimika kuingilia kati baada ya kuzuka mapigano kati ya wafuasi
na wapinzani wa Mohamed Morsi Rais halali wa nchi hiyo aliyepinduliwa na jeshi
huko Mansoura katika kaunti ya Dakhlia.
Mapigano hayo
yalitokea jana wakati pande mbili hizo zilizokuwa kwenye maandamano tafauti
katika Chuo Kikuu cha al Mansoura kuanza kurushiana mawe.
Polisi wa kutuliza
ghasia waliingilia kati mapigano ya wapinzani na wafuasi wa Morsi kwa
kuwanyunyizia gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya.
Hata hivyo hadi
sasa hakuna ripoti iliyotolewa juu ya watu waliouawa au kujeruhiwa kwenye
ghasia hizo huko Mansoura.
Misri imekuwa
ikishuhudia ghasia na mapigano kati ya wafuasi na wapinzani wa Morsi katika
maeneo kadhaa ya nchi hiyo tangu kupinduliwa na jeshi, rais huyo halali mwezi
Julai mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment