Umoja wa wanawake wa
taasisi ya center for training and development initiative, CENTRADIN, wamelaani
vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika mchakato unaoendelea hapa
nchini wa kupata katiba mpya.
Akitoa tamko jijini DSM
kuhusu mchakato wa amani katika kupata katiba mpya mkurugenzi mtendaji wa
taassi hiyo kwa niaba ya wanawake wa umoja huo, SAUM RASHIDY amewaeleza
waandishi wa habari kuwa uvunjifu wa amani ukitokea watakaoathirika ni
wanawake, wazee, walemavu na watoto na kuongeza kuwa katiba haiwezi kupatikana
kwa maandamano na vurugu ila kwa maridhiano ya kitaifa.
Aidha katika kuendeleza
amani na maridhiano ya kitaifa wameomba viongozi wa vyama vya siasa na rais
wakutane na kukubaliana juu ya mustakabali mzima wa kupata katiba nzuri na ya
watanzania wote pamoja na kudumisha amani.



0 comments:
Post a Comment