Gaudensia Kabaka - Waziri wa kazi na ajira Tanzania.
Waziri wa kazi na ajira
Gaudensia Kabaka amewataka waajiri nchini kuwapa uhuru wafanyakazi wao wa
kuchagua mifuko ya hifadhi za jamii wanayoitaka kutokana na faida
watakazozipata badala ya kuwalazimisha kujiunga na mfuko mmoja wanaoutaka
waajiri.
Akifunga mkutano mkuu
wa sita wa mwaka wa mfuko wa pension wa LAPF jijini arusha waziri kabaka
amesema katika marekebisho ya sheria namba 5 ya mwaka 2012,mifuko inapaswa
kumtambua mdhibiti wa mifuko na kwamba mifuko hiyo ni kwa watanzania wote bila
kuchagua anafanyakazi sehemu gani.


0 comments:
Post a Comment