Idara ya uhamiaji
nchini imesema imefanikiwa kudhibiti hati na vibali bandia vilivyokuwa vikitolewa
na matapeli kwa wageni wanaoingia nchini baada ya kuanzisha utoaji vibali kwa
njia ya kieletronic ambavyo vimewekwa alama nyingi za usalama ambazo sio rahisi
kuzinakili.
Mrakibu Mwandamizi anayeshughulikia utoaji wa vibali kwa wageni wanaoingia
nchini Bw,Philon fabian ketema amesema utaratibu huo ulioanzishwa mwezi june
mwaka huu umesaidia kudhibiti vibali feki vya ukaazi ambavyo vilikuwa
vikisababisha upotevu wa mamilioni ya fedha serikali.
Katika
kuhakikisha Uhamiaji inapambana na udanganyifu pamoja na vitendo vya rushwa kwa
baadhi ya watumishi wa idara hiyo ,Idara
hiyo imeanzisha uombaji visa,passport kwa njia ya mtandao ambapo mwombaji mara
atakapokamilisha taratibu anatakiwa kulipipia kwa njia ya benki tofauti na
awali.


0 comments:
Post a Comment