Rais Uhuru Kenyatta wa
Kenya.
Rais Uhuru Kenyatta wa
Kenya amerejea nyumbani baada ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Afrika
mjini Addis Ababa, Ethitopia ambao umeazimia kwa kishindo kwamba yeye na Naibu
wake William Ruto, wasionekane kwenye mahakama ya Kimataifa ya uhalifu - ICC.
Mkutano huo wa Wakuu wa
nchi za Afrika ulikuwa chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu wa Ethiopia Haile
Mariam Dessalgn ambapi ulijadili kwa kina uhusiano wa Mahakama ya Kimataifa ya
Uhalifu - ICC na bara la Afrika.
Wazungumzaji katika
Mkutano huo wamelitakata Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na ICC
kushirikiana na Umoja wa Afrika, kuhakikisha uongozi wa Kenya unatekeleza
majukumu yake ya kikatiba.


0 comments:
Post a Comment