Jim Yong
Rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim ameonya kwamba Marekani
imebakisha siku chache tu kabla ya kuingia kwenye hatari kubwa kwa sababu ya
mgogoro wa Serikali ya nchi hiyo kukopa.
Amewataka watunga sera wa Marekani kufikia makubaliano ya
kuongeza kiwango cha ukopaji cha Serikali ya nchi hiyo kabla ya siku ya Alhamisi ijayo.
Hazina ya Marekani itaanza kufilisika iwapo hakuna
makubaliano kwa serikala ya Marekani kukopa kwenye masoko ya fedha.Bwana Kim
ameonya kuwa hili linaweza kuwa janga la dunia pia.
Amesema kadri Marekani inavyozidi kushindwa kutoa maamuzi ya
haraka, hali itakuwa mbaya zaidi kwa nchi zinazoendelea, ambapo amesema viwango vya riba vitaongezeka,
imani itapungua na ukuaji wa uchumi utapungua kasi yake.


0 comments:
Post a Comment