Watu wasiopungua 20 wamefariki dunia na wengine 23
hawajulinaki walipo kufuatia ajali ya meli iliyotokea karibu na Mopti, mji wa
katikati mwa Mali.
Idara ya ulinzi wa usalama wa umma mjini humo imetoa
taarifa ikisema, watu 210 wamenusurika, na idadi ya waathiriwa huenda
ikaongezeka wakati shughuli za uokoaji zinapoendelea.
Habari zinasema abiria wengi wa mashua hiyo walikuwa
wakielekea vijijini mwao kwa ajili ya sikukuu ya kiislamu ya Tabaski Jumanne
ijayo.
Nahodha mmoja wa mashua amesema, ajali hiyo huenda
ilisababishwa na ubebaji abiria wengi kupita kiasi.


0 comments:
Post a Comment