Image
Image

MISRI YATANGAZA NIA YA KUANZISHA TENA MRADI WA NISHATI YA NYUKLIA NCHINI HUMO.




Rais wa serikali ya mpito ya Misri Adly Mansour ametangaza nia ya kuanzisha tena mradi wa nishati ya nyuklia nchini humo.

Tangazo hilo la Mansour limezua matumaini ya kufikiwa kwa ndoto ya mradi wa nyuklia nchini Misri.

Hata hivyo kuna baadhi ya watu wanaopinga mradi huo kutokana na kuwepo kwa nishati endelevu kama vile nishati ya jua na upepo.

 Aidha Wengine pia wanatilia shaka uwezo wa Misri kukamilisha mradi huo wakati inapokumbwa na msukosuko wa kisiasa na matatizo ya kiuchumi.

 Akizungumza na shirika la habari la China Xinhua, mwenyekiti wa zamani wa kituo cha kitaifa cha usalama wa nyuklia nchini Misri Bw Karim al-Adham amesema Misri inahitaji sana mradi huo kutokana na upungufu wa umeme na kupungua kwa visima vya mafuta nchini humo.

 Mwaka wa 2006, Misri ilitangaza kufufua mpango wa nishati ya nyuklia kwa raia katika eneo la el-Dabaa kilomita 150 magharibi mwa mji wa Alendandria, lakini wakazi wa huko walifika na kuharibu miundo mbinu ya mradi huo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment