Image
Image

UTAPIA MLO WASABABISHA VIFO 362 VYA WATOTO HUKO NIGER.




Ripoti za Umoja wa Mataifa zimeeleza kuwa, zaidi ya watoto 360 walio na umri wa chini ya miaka mitano wamefariki dunia nchini Niger kutokana na utapiamlo.  

Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa mjini Niamey amesema kwamba, vifo hivyo vya watoto wadogo vilitokea kati ya mwezi Januari na Septemba mwaka huu katika eneo la Zinder.

Eneo hilo lenye watu wengi na masikini la Niger mara kwa mara linakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na ukame, tatizo ambalo linawaathiri zaidi wanawake na watoto.

 Kwa mujibu wa  Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF utapiamlo unasababishwa na ukosefu wa virutubisho muhimu katika miili ya watoto, tatizo linalochelewesha ukuaji na kudhoofisha mfumo wa kinga mwilini dhidi ya magonjwa ya kawaida ya utotoni.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment